RUVU SHOOTING:TUNA ASILIMIA NYINGI KUSHINDA MBELE YA YANGA

AMBROSE Morris, nahodha wa Ruvu Shooting ameweka wazi kuwa wana asilimia nyingi za kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Itakuwa ni saa 12:15 jioni mchezo huo wa kukata na mundu unatarajiwa kuanza huku viingilio ikiwa ni 5,000 mzunguko,10,000 VIP B na VIP A itakuwa ni 15,000.

Akizungumza na Saleh Jembe, nahodha huyo aliweka wazi kuwa wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wamejipanga kuona kwamba wanashinda mchezo huo muhimu.

“Kwanza kabisa tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha Dar salama kwa kuwa tumesafiri umbali mrefu kutoka Mlandizi na sasa tupo hapa kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho.

‘Tuna asilimia nyingi za kushinda mbele ya Yanga na tunajua kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini sisi tupo tayari hivyo hakuna mashaka ambayo tunayo kwa wakati huu kutokana na mbinu ambazo tumepewa.

“Ukweli ni kwamba asilimia nyingi huwa zinaanzia mbili,sita 10 mpaka 50 hivyo sijasema kwamba tuna asilimia 100 ya kushinda hapana. Kila kitu kinakwenda sawa na mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Jambo ambalo ninaweza kuwaambia mashabiki wetu wa Ruvu Shooting ni kwamba maandalizi yetu yapo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa hivyo wajitokeze kwa wingi kuwa nasi kwenye mchezo wetu,”.