
Sports


VIDEO:MWENYEKITI WA SIMBA AFUNGUKIA ISHU YA USAJILI
MWENYEKITI wa Simba, Murtanza Mangungu ameweka wazi kuwa wachezaji wa Simba wanajitambua na hakuna ambaye atafanikiwa kuwatoa mchezoni wachezaji kutokana na masuala ya usajili.

YANGA YATENGA DAKIKA 90 ZA KUANDAA KIKOSI KAZI
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utatumia dk 90 kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Mafunzo kwa ajili ya kuandaa kikosi kazi kitakachomenyana na Azam FC. Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imekusanya pointi 48 ikiwa nafasi ya kwanza inatarajiwa kumenyana na Azam FC iliyo nafasi ya 3 na pointi 28 zote zimecheza…

NYOTA YANGA PRINCESS SAFARI ULAYA IMEIVA
MCHEZAJI wa Yanga Princess na Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars Asha Masaka leo Machi 30,2022 ameanza safari kuelekea Sweden. Mshambuliaji huyo anakwenda kuanza changamoto mpya za maisha katika Klabu ya BK Hacken ya nchini Sweden. Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Sweden itakuwa na nyota huyo mzawa ambaye alikuwa ni chaguo…

MTAMBO WA MABAO YANGA HATIHATI KUIKOSA AZAM
IMEFAHAMIKA kuwa, kiungo tegemeo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amepata majeraha yaliyomfanya aondolewe kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, hivyo kuna uwezekano mkubwa akaikosa mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam itakayochezwa Aprili 6, mwaka huu. Kwa sasa Taifa Stars ipo kambini kwa ajili ya kucheza mechi za…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatano

MKATABA WA NBC NA TFF KUWA NA TIJA KWA FAMILIA YA MICHEZO
LEO Machi 29, benki ya NBC ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Bara ya Tanzania wameingia makubaliano na Shirikisho la Mpira Tanzania kwa ajili ya Bima ya Afya na maisha. Makubaliano hayo ni maalumu ambapo TFF imeweza kuingia na NBC ili kuweza kutoa bima za afya kwa familia ya michezo. Bima hizo za afya zinatarajiwa…

TAIFA STARS KAZINI LEO,FEI TOTO KUIKOSA SUDAN
KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo Jumanne kitacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Sudan kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema vijana wake wapo vizuri kukabiliana na wapinzani wao. Mchezo huu unakuja baada ya…

ISHU YA MAYELE KUSEPA YANGA YAFAFANULIWA
UONGOZI wa Yanga umefunguka ishu ya mshambuliaji wao wa kati kipenzi cha mashabiki, Fiston Mayele kuhusishwa kujiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Yanga wametoa tamko rasmi kuwa mzee huyo wa kutetema hataondoka kutokana na kuwa na mkataba wa kuendelea kukipiga ndani ya klabu hiyo. Mayele kwa sasa ndiye mshambuliaji tegemeo wa Yanga akiwa ndiye…

PABLO APIGA HESABU ZA USHINDI,SAKHO,DILUNGA MAJANGA
PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya US Gendarmerie unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Simba iliyo nafasi ya tatu ina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu ili kuweza kukata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali. Tayari kikosi kipo kambini kwa ajili ya maandalizi…

USHINDI MKUBWA KWENYE KASINO YA MERIDIANBET!!
Kwa muda mrefu sasa, unapoizungumzia Kasino ya Meridianbet, unazungumzia Jakipoti za Kasino na ushindi mkubwa! Kwa mwaka 2022 pekee, mpaka sasa kuna washindi wawili wametusua ushindi mkubwa!! Mchezaji mwingine wa Kasino kupitia Meridianbet alijaribu bahati yake kupitia mchezo wa Crazy Time unaotengenezwa na kampuni ya Evolution. Gurudumu lenye maajabu ya kusaka pesa lilifanya kazi…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne

RS BERKANE WAPIGWA FAINI NA CAF KISA SIMBA
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika, CAF imeipiga faini Klabu ya RS Berkane kutokana na vitendo visivyo vya kinidhamu kwenye mechi za Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba. Taarifa iliyotolewa mapema leo Machi 28 na CAF imeeleza kuwa mechi iliyochezwa Februari 2022, Simba wakiwa ugenini, mashabiki wa RS Berkane waliwashambulia wachezaji wa Simba…

BANDA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA
KIUNGO wa Simba, Peter Banda ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki kwa mwezi Machi. Banda ameweza kushinda tuzo hiyo akiwazidi kura nyota wawili ambao aliingia nao katika fainali inayodhamiwa na Emirate Aluminium. Nyota hao ni pamoja na beki wa kazi ngumu na chafu Shomari Kapombe pamoja na kiungo wa kupekecha Pape Sakho. Kapombe aliweza…

MTAMBO WA MABAO YANGA KUREJEA KAZINI
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Yacouba Songne anaweza kurejea uwanjani muda wowte kuanzia sasa baada ya kuwa nje kwa muda akitibu goti. Yacouba aliumia katika mchezo dhidi ya Geita Gold Oktoba 2, mwaka jana ambao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jesus Moloko ambapo yeye alitoa pasi ya bao hilo. Daktari wa Yanga, Youssef…

BODABODA 8 KUWA MIKONONI MWA WATANZANIA KUTOKA HALOPESA
KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania ya Halotel Tanzania,leo Machi 28 imezindua promosheni ya ‘Shinda na Halopesa’ itakayotoa fursa kwa wateja kuweza kushinda fedha taslimu pamoja na Pikipiki maarufu kama ‘Bodaboda’ mpya kabisa. Promosheni hii itadumu kwa muda wa wiki 8 ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa na ni jumla ya wateja 72 watashinda zawadi mbalimbali zitakazotolewa…

CHELSEA YAPIGA 9-0 LEICESTER
TIMU ya Wanawake ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya timu ya Wanawake ya Leicester City. Mchezo huo wa Ligi ya Wanawake ulichezwa Uwanja wa The King Power Jumapili ya Machi 27,2022. Mabao ya Guro Reiten ambaye alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 3 na 45+5 huku Sam Kerr yeye alitupia mawili…