YANGA:TUNAZIDI KUIMARIKA

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kwamba kikosi hicho kinazidi kuimarika taratibu kutokana na mechi ambazo wanacheza. Mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga haijapoteza mchezo kwenye ligi na inaongoza ligiikiwa na pointi 32. Jana Januari 18, Yanga ilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC ambapo iliweza kushinda mabao 2-0…

Read More

KOCHA YANGA AMTAJA MSHERY

KOCHA mpya wa makipa wa Yanga, Mbrazili, Milton Nienov amefunguka kuwa usajili wa kipa, AboutwalibMshery ni usajili bora kufanywa na klabu hiyo kutokana na ubora wake, Kocha huyo ameweka wazi kuwa ameanza na suala la kuhakikisha makipa wa timu hiyo wanahimili presha ya michezo mikubwa. Milton alitambulishwa rasmi na Yanga Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo alikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga huku Yanga…

Read More

JEMBE LA KAZI TAYARI KUREJEA SIMBA

BAADA ya mwishoni mwa mwaka jana taarifa kusambaa kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kuvunja Mkataba wake na Kiungo Mganda Taddeo Lwanga baada ya kupata majeraha uongozi umetaja siku atakayorejea kikosini. Mashabiki wataweza kumuona kwa mara nyingine tena kiungo huyo wa kazi chafu mwishoni mwa Januari hii kwa mujibu wa Ofisa Habari, Ahmed Ally….

Read More

RATIBA YA LEO LIGI KUU BARA

LIGI Kuu Tanzania Bara bado inaendelea na leo Januari 20 kutakuwa na mchezo mmoja kwa timu kusaka pointi tatu muhimu. Mbeya City ambayo imetoka kutibua rekodi za Simba kwa kuwatungua kwenye mchezo uliopita Januari 17 kwa bao 1-0 leo itamenyana na Ruvu Shooting. Mbeya City iliweza kusepa na pointi tatu mazima kwa ushindi huo na…

Read More

KOCHA AZAM FC AIBUKIA BIASHARA UNITED

BIASHARA United imemtambulisha rasmi Vivier Bahati kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na tayari ameanza kazi rasmi kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara. Bahati alikuwa anainoa timu ya Azam FC mkataba wake ulivunjwa kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo na waliondoka pamoja na Kocha Mkuu, George Lwandamina. Anachukua mikoba ya Patrick Odhiambo ambaye…

Read More

FT:MBUNI FC 0-2,MUKOKO ATUPIA MBILI

UWANJA wa Sheikh Amri Abeid dakika 90 zimekamilika kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mbuni ambapo ni Yanga wameibuka kidedea kwenye mchezo wa leo. Mabao yote ya Yanga yamefungwa kipindi cha pili kwa kuwa dakika 45 za mwanzo timu zote zilitoshana nguvu na mtupiaji ni Mukoko Tonombe ambaye alifunga mabao hayo kwa penalti…

Read More

MCHEZO WA KIRAFIKI, YANGA 0-0 MBUNI FC

MCHEZO wa kirafiki kati ya Yanga v Mbuni kwa sasa ni mapumziko Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mchezaji wa Mbuni Hussein Idd ameonyeshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Yanga David Bryson. Kiungo mshambuliaji Dickosn Ambundo alifanya jaribio la kwanza na matata kwa upande wa Yanga lakini liliokolewa na kipa…

Read More

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBUNI FC

LEO kikosi cha Yanga kinacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania. Hiki hapa kikosi cha kwanza:- Johora Boxer Bryson David Mukoko Ibrahim Bacca Zawad Mauya Sure Boy Ambundo Farid Mussa Kaseke Makambo Benchi Magaigwa Job Balama Moloko…

Read More

YANGA KUTESTI MITAMBO LEO

VINARA wa Ligi Kuu Bara Yanga leo watakuwa na kazi ya kutesti mitambo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC. Saa 10:00 jioni mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ikiwa ni kwa ajili ya hesabu za mchezo wao ujao dhidi ya Polisi Tanzania ambao ni wa ligi. Januari 23 Yanga yenye…

Read More

SIMBA KITUO KINACHOFUATA MANUNGU

BAADA ya kurejea Dar wakitoka Mbeya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kituo chao kinachofuata ni Manungu. Chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco, Januari 17,2022 alishuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine ukisoma Mbeya City 1-0 Simba na mtupiaji alikuwa ni Paul Nonga dakika ya 19. Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hiyo kupoteza ndani…

Read More

AZAM WASEPA NA POINTI TATU ZA MBEYA KWANZA

Rodgers Kola amepachika bao mbele ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine. Bao hilo la ushindi amelipachika kimiani dakika ya 44 katika kipindi cha kwanza. Jitihada za Mbeya Kwanza kuweza kuweka mzani sawa ziligonga mwamba katika dakika 45 za kipindi cha kwanza. Hata kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu…

Read More

MORRISON AFUGUKIA ISHU YA KUSUGUA BENCHI

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa, hana shida na kuanzia benchi ndani ya kikosi hicho, kwani ni jambo la kawaida kwenye timu yoyote kubwa na wajibu wake kama mchezaji ni kuhakikisha anaongeza jitihada kumshawishi kocha kumpa nafasi. Tangu kiungo raia wa Senegal, Pape Sakho aanze kuuwasha moto ndani ya Simba, Morrison ameonekana kupata…

Read More

SIMBA YATAJA TIMU ITAKAYOTWAA UBINGWA

KOCHA wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa kwa upande wako anaona Azam FC wanayo nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa siku za mbeleni kutokana na kikosi chao kuimarika kila siku. Pablo amesema amekutana na Azam FC kwenye mechi mbili kwa siku za hivi karibuni na ameona kuna utofauti mkubwa kwenye mechi ya kwanza na ya pili ambayo wamecheza na anaona kabisa timu ina ari ya…

Read More