MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi
Baada ya purukushani za wiki 37, hatimaye bingwa wa EPL na Serie A kujulikana kwenye wiki ya 38. Nani ataibuka kidedea? Mchongo upo Meridianbet. Inter Millan watakua San Siro wakichuana na Sampdoria. Ni tofautui ya alama 1 kati yao na majirani zao, AC Milan. Pointi 3 ni muhimu kwa timu zote, Inter watafanikiwa kutetea…
VINARA wa Ligi Kuu Bara leo wamesepa na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Mbeya Kwanza ya Mbeya. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 63 ikiwa inazidi kuukaribia ubingwa wa ligi msimu wa 2021/22. Ni mabao ya Fiston Mayele ambaye ametupia bao la kufungulia kwa Yanga dk ya 34 kisha msumari wa pili…
NDANI ya dakika 45, Yanga imefunga mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaochezwa Uwanja wa Mkapa. Kasi walianza nayo ndani ya dakika 15 kwenye mchezo huo huku Mbeya Kwanza wakiwa kwenye mbinu ya kujilinda zaidi kwenye mchezo wa leo. Ni mabao ya Fiston Mayele ambaye ametupia bao la kufungulia…
SAA 1:00 leo Mei 20,2022 Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili. Ni kikosi kamili Yanga wameanzisha mbele ya Mbeya Kwanza ikiwa namna hii:- Diarra Djigui Kibwana Shomari Farid Mussa Yannick Bangala Dickson Job Khalid Aucho Sure Boy Jesus Moloko Ambundo Ntibanzokiza Mayele…
LEO Mei 20,2022 Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ametangaza orodha ya wachezaji wa timu hiyo watakaoingia kambini. Wachezaji hao ambao wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitaingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2023 wana kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi mbili za awali. Kwa upande…
MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Mei 20 umeendelea ambapo mechi mbili zimekamilika kwenye viwanja viwili tofauti. Mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ubao umesoma Coastal Union 2-1 Dodoma Jiji. Mabao ya Coastal Union mtupiaji ni kijana Abdul Suleiman aliyeanza kuwatungua Dodoma Jiji dk 7 na 15 lile la Dodoma Jiji ni…
KLABU ya Simba ipo katika mazungumzo na beki la kazi raia wa Cameroon, Jean Jospin Engola kwa ajili ya kuimarisha ukuta wa timu hiyo kuelekea msimu ujao. Simba huenda ikaachana na mabeki wake wa kati akiwemo Pascal Wawa na Erasto Nyoni, hivyo ipo katika mawindo ya kusajili beki mwingine wa kimataifa kuziba nafasi hiyo. Akizungumza…
LEO vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanatarajiwa kucheza na Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa ligi, hiki hapa kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuanza
KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars leo Mei 20 ametangaza kikosi cha timu ya Taifa ambacho kitaingia kambini kwa ajili ya mechi za kuwania Kufuzu AFCON
PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema wapinzani wao Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali haiwapi presha kwa kuwa wanaamini watafanya maandalizi mazuri. Zimebaki siku 7 kabla ya watani hawa wa jadi hawajakutana kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mei 28. Pablo amesema kuwa anawatambua wachezaji wake namna…
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mshambuliaji wake namba moja Fiston Mayele atafunga kwenye mechi zilizobaki kwa kuwa anapenda kufunga na uwezo anao. Mayele kwenye mechi nne mfululizo za ligi hajafunga akiwa ameachwa kwa bao moja na mtupiaji namba moja George Mpole wa Geita Gold mwenye mabao 13 na pasi tatu za mabao….
OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez atafikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa ushahidi wa shutuma anazodaiwa kuzitoa wakati akihojiwa na Kituo cha Radio nchini Afrika Kusini hivi karibuni. Katika taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa, Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko yao kwa TFF dhidi ya…
CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza ambao unatarajiwa kuchezwa leo Mei 20, Uwanja wa Mkapa. Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi zao 60 baada ya kucheza mechi 24 wanakibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya Kwanza ambao…
MCHAMBUZI wa Soka Saleh Ally ‘Jembe’ katika kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na 255globaradio na Global TV amesema kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia Rally Bwalya amekuwa kwenye kiwango ambacho hakieleweki kwa kukipa tafsiri ya maji kupwa maji kujaa. Jembe amesema kwamba kuna muda anakuwa katika kiwango kizuri na muda mwingine anakuwa kwenye kiwango…
USHINDANI unazidi kuwa mkubwa kila iitwapo leo hivyo nafasi inapopatikana ni lazima kufanya kweli bila kuogopa. Kila kitu kinawezekana na muda wa kufanya hivyo ni sasa baada ya kuwa kwenye kazi ngumu kutimiza kwenye mechi ambazo walianza awali kucheza na kupata ushindi. Ni timu ya Taifa ya Wasichana U 17 ambayo inapeperusha bendera ya Tanzania…
MWENDO unazidi kusonga kwa sasa kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni lala salama ya moto na yenye ushidani mkubwa. Wakati wa kupanda kile ambacho ulikuwa unastahili ni sasa na ambaye ataweza kushinda atacheka na yule ambaye atashindwa tabasamu litayeyuka kwake. Huu ni mzunguko ambao unakwenda kuamua nani anakuwa bingwa na nani anakwenda…