KIUNGO wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Abdul Suleiman, ‘Sopu’ yupo chini ya uangalizi wa madaktari ili kuweza kurejea kwenye ubora wake.
Kiungo huyo ni mali ya Azam FC alipata maumivu akiwa na timu yake ya Azam baada ya kurejea kutoka Misri walipokuwa wameweka kambi.
Kiungo huyo ni miongoni mwa nyota walioitwa na Kim Poulsen kuikabili Uganda kwenye mchezo wa CHAN unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 28.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Cliford Ndimbo amesema kuwa wachezaji wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.
“Wachezaji wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wapo tayari isipokuwa Sopu, (Abdul Suleiman) yeye yupo chini ya uangalizi maalumu wa madkatari.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao na hasa ukizingatia viingilio ni 5,000 na 2,000 kwa mzunguko,” amesema Ndimbo.