SIMBA QUEENS YAFANYA KWELI KIMATAIFA

USHINDI wa mabao 5-1 dhidi ya AS Kigali umewapa nafasi Simba Queens kutinga hatua ya Fainali Ligi ya Wanawake Afrika Ukanda wa CECAFA.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex timu zote zilikuwa zinasaka ushindi ili kuweza kupata matokeo na kuweza kusonga mbele.

Shukrni kwa mabao ya Vivian Carozone aliyefunga mawili, Opah Clement alitupia bao moja, Aisha Juma alitupia bao moja na Diana William alitupia bao moja.

Mabao hayo yaliwapa Simba nguvu ya kuweza kuendelea kulinda ushindi wao na kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Bao la wapinzani AS Kigali ambalo ni la kufuta machozi limefungwa na Mukeshimana Dorothe.