NYOTA wa zamani wa Yanga, Said Ntibanzokiza anatajwa kumalizana na Klabu ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Nyota huyo ambaye alijenga pacha matata na Fiston Mayele alisepa ndani ya kikosi hicho mwishoni mwa msimu wa 2021/22 baada ya kandarasi yake kugota ukingoni.
Ni dili la miaka miwili anatajwa kupewa nyota huyo ambaye ni mtaalamu kwenye mapigo ya mipira iliyokufa.
Taarifa zinaeleza kuwa tayari wamefikia makubaliano mazuri na nyota huyo kilichobaki ni kuweza kutambulishwa ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro.
Alipokuwa Yanga alifunga mabao 7 kwenye mechi 17 za ligi ambazo alicheza hivyo anakwenda kuongeza kasi kwenye kiungo ndani ya Geita Gold.