UONGOZI wa Geita Gold umeweka wazi kuwa makubaliano ya kuachana na wachezaji wao yamezingatia utaratibu kwa kuwa wanaheshimu mikataba ya wachezaji wao.
Timu hiyo imetangaza kuachana na wachezaji saba na kufikisha idadi ya wachezaji 9 ambao wameondoka katika kikosi hicho.
Wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya Geita Gold ni pamoja na Maka Edward, Ramadhan Athuman Teleza, Pius Luchagila, Makezi Ramadhan, Willian Luccian Gallas, Venacne Ludovic na Hassan Ramadhan wengine ni Juma Nyoso na Khomen Aboubhakari ambao wamepata changamoto mpya.
Staa mwingine ni Ditram Nchimbi ambaye alijiunga na timu hiyo msimu wa 2021/22 akitokea Yanga lakini hakuweza kucheza zaidi ya mechi tano.
Mratibu wa Geita Gold, Mpambayange Abdalah amesema kuwa iliwachukua muda kuachana na wachezaji kutokana na taratibu.
“Wachezaji ambao tumeachana nao ilikuwa ni lazima kufanya nao mazungumzo na tumefuata utaratibu kwa kufuata sheria ili haki iweze kupatikana hasa ukizingatia kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake,” amesema Mpambayange.