AZAM FC KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA

KIKOSI cha Azam FC kinatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Djibout, AS Arta Solar 7, mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex Agosti 30 mwaka huu saa 1.00 usiku.

Timu hiyo imesajili nyota wa zamani waliowika kwenye Ligi Kuu England, Alex Song na Solomon Kalou.

Azam FC ilifanya maandalizi yake nchini Misri kwa kuweka kambi huko kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.

Baada ya kurejea Bongo ilifanya tamasha lake maalumu la utambulisho wa wachezaji wake wapya pamoja na wale wa zamani ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Pascal Mshindo, Tepsi Evance huku wapya ikiwa ni pamoja Abdul Suleiman kiungo aliyekuwa anakipiga Coastal Union.

Kwenye ligi imecheza mechi mbili na kukusanya pointi nne, imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Kagera Sugar na kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold.