FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amebainisha wazi kuwa makosa ambayo wameyafanya kwenye mechi mbili mfululizo watayafanyia kazi ili waweze kurejea wakiwa imara.
Timu hiyo kwenye mechi mbili za ligi msimu wa 2022/23 imeyeyusha pointi sita mazima kwa kuwa ilifungwa kwenye mechi hizo.
Ilianza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex na mabao 2-0 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.
Baraza amesema: “Tulipoteza mchezo wa kwanza ugenini mbele ya Azam FC kisha tukapoteza mchezo wa pili dhidi ya Simba, makosa ambayo tumefanya tutayafanyia kazi ili tuweze kuwa imara.
“Tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inapata ushindi nasi tunahitaji kuona inakuwa hivyo, wakati unakuja tutakuwa imara,” amesema.
Kwa sasa ligi imesimama mpaka Septemba 6 kupisha mashindano ya CHAN ambapo timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza na Ugandana wacjhezaji wameingia kambini.