KIKOSI cha kwanza cha Simba kitakachoanza dhidi ya Yanga mchezo wa Ngao ya Jamii leo Agosti 13 langoni kipa namba moja Aishi Manula amekosana hivyo makujukumu yapo kwa Beno.
Maki Zoran Kocha Mkuu wa Simba ameanza namna hii ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ushindani ndani ya kikosi cha Simba:-Beno Kakolanya, Israel Mwenda, Mohamed Hussein,Henock Inonga, Mohamed Quattra, Jonas Mkude, Pape Sakho,Sadio Kanoute,Habib Kyombo,Clatous Chama na Kibu Denis
Akiba ni Ally,Shomary Kapombe, Joash Onyango, Victor Akpan,Okraha,Mzamiru Yassin,Dejan, John Bocco na Okwa.