TAIFA STARS YAPOTEZA KWA MKAPA

IKIWA uwanja wa Mkapa leo Novemba 11, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya DRC Congo.

Ilikuwa ni katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo Stars ilikuwa inapambana kupata pointi tatu sawa na DRC Congo.

Kipindi cha kwanza umakini kwa safu ya ushambuliaji ya Stars inayoongozwa na Mbwana Samatta ulikuwa mdogo na kufanya wakose nafasi za wazi.

Kituo kinachofuata ni Madagascar ambapo utakuwa mchezo wa mwisho kwa kundi J katika kuwanja kufuzu Kombe la Dunia.

Kwa hesabu hizo Tanzania imeondolewa katika Vita ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa kuwa inabaki na pointi 7 huku DRC Congo ikifikisha pointi 8 na kinara ni Benin ni namba moja ikiwa na pointi 10.