BAADA ya kikosi cha Azam FC kurejea Agosti 8 kutoka Misri ambapo kilikuwa kimeweka kambi,leo Agosti 9 wachezaji wa timu hiyo wanatarajiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.
Azam FC ilikuwa ni timu ya pili kutoka Tanzania kuweka kambi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.
Ilianza Simba ambayo tayari ipo Bongo iliwahi kurejea mapema kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day iliyofanyika Agosti 8 pamoja na mchezo wao ujao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Azam FC wao wanakuja na tamasha lao la kipekee ambalo wamelipa jina la AZAMKA.
Tamasha hilo ambalo litaratibiwa na mashabiki kwenye kila jambo linatarajiwa kufanyia Agosti 14, Uwanja wa Azam Complex.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa siku hiyo mashabiki watakutana na kupanga kila kitu wenyewe kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi.
“Tutacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zesco United huu utakuwa ni mchezo wa tatu kwa timu hizi kukutana kwenye mechi za kirafiki.
“Ninawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwani hii ni siku yao wenyewe wanapaswa wafurahie zaidi,” amesema.