NABI APIGA HESABU ZA NGAO YA JAMII DHIDI YA SIMBA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kupoteza mchezo wa kimataifa dhidi ya Vipers SC ni njia kwake kuweza kushinda Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 Agosti 6,2022 Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Vipers ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Simba,Agosti 13, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kirafiki wa kimataifa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo ilikuwa ni siku maalumu ya utambulisho wa uzi mpya pamoja na wachezaji wa kikosi cha 2022/23.

Nabi amesema:”Hata msimu uliopita tulikutana na mambo kama haya lakini kikubwa ilitokana na kuwa na muda mfupi wa kufanya maandalizi hilo tunalijua na tutalifanyia kazi ili kuwa imara.

“Ninafahamu ukubwa na ugumu wa mechi ila kwetu ushindi ni muhimu na una maana kubwa kwamba tutaweza kufanya vizuri msimu ujao hivyo bado tuna nafasi na makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba,” amesema.

Msimu wa2021/22 Ngao ya Jamii ilikuwa mali ya Yanga baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba hivyo mchezo ujao wanakwenda kutetea taji lao la kwanza kwa msimu mpya wa 2022/23.