AZAM FC WAJA NA AZAMKA

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa msimu huu wanakuja tofatauti katika tamasha lao ambapo litakuwa mikononi mwa mashabiki.

 Thabit Zakaria,Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa watakuwa na tamasha maalumu linalokwenda kwa jina la AZAMKA ambalo ni kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wao lakini watakaoandaa mpango kazi ni mashabiki wa Azam FC.

Kwa sasa Azam FC imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 chini ya Kocha Mkuu,Abdi Hamid Moallin.

“Tutakuwa na tamasha maalumu ambalo litawapa fursa mashabiki kuweza kujuika na timu yao na itakuwa ni Agosti 14 na kutakuwa na mechi ya kirafiki pia.

“Siku hiyo itakuwa ni siku ya mashabiki wenyewe kuweza kupanga kila kitu wale wenye uwezo wa kuimba na kutunga mashairi,wale wenye uwezo wa kucheza itakuwa hivyo waunde timu zao waje wenyewe,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Azam FC ni pamoja na Abdul Suleiman,’Sopu’ Cleoface Mkandala.