KIPA wa mpira Mohamed Makaka atakuwa ndani ya Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2022/23 baada ya kupata dili jipya kwa mabosi hao ambao makao yao makuu ni Morogoro.
Alikuwa ni kipa namba moja ndani ya Ruvu Shooting ambapo alikuwa hapo msimu wa 2021/22.
Unakuwa ni usajili wa tatu kwa Mtibwa Sugar kuweza kutambulisha baada ya kuanza na Charlse Ilanfya ambaye alikuwa anacheza KMC pamoja na Idd Mobby.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ameweka wazi kuwa watafanya usajili mzuri kwa ajili ya kuweza kuleta ushindani ndani ya ligi.
“Tunahitaji kuwa na kikosi imara na bora ambacho kitaleta ushindani,kikubwa ni kuona kwamba kila mmoja anfanya vizuri na hasa ukizingatia kwamba hatukuwa na msimu bora,” amesema.
Baadhi ya wachezaji wameondoka hapo ikiwa ni pamoja na Jaffary Kibaya,Ibrahim Ame na Salum Kihimbwa.