MSUVA APATA TIMU MPYA

NYOTA mzawa Simon Msuva ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kuweza kuanza changamoto mpya katika Klabu ya Alqadsiah ya Saudi Arabia.

Winga huyo hakuwa na timu kwa muda kutokana na kushughulikia kesi yake FIFA kuhusu mkataba wake na malipo na mwisho wa siku aliweza kushinda.

Alikuwa anatajwa kuweza kurejea ndani ya klabu yake ya zamani Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na mazoezi yake alikuwa anafanyia kwenye kituo cha Cambiasso.

Pia Shirikisho la Soka Tanzania, TFF limeweza kumtakia kila la kheri  kwa kupata changamoto mpya kwenye klabu hiyo mpya ambayo inashiriki Ligi Daraja la pili.

Msuva amejiunga na klabu hiyo ya daraja la pili ya Saudi Arabia kutoka kwa Mabingwa wa Afrika ambao ni Wydad Casablanca walioshinda kwenye fainali mbele ya Al Ahly ya Misri ambapo alisitisha mkataba na timu iliyotwaa ubingwa wa Afrika.