INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba, Mohamed Ouattara amebainisha kuwa alifuatilia malengo ya timu hiyo na kuweza kukubali kusaini katika timu hiyo.
Kapewa dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Simba ambayo inanolewa na Kocha Mkuu Zoran Maki raia wa Serbia.
Beki huyo amebainisha kwamba anamatumaini makubwa ya kuweza kufanya vizuri ndani ya timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara,Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mohamed amesema:”Niliweza kuifuatilia Simba kwa muda na kuona namna ilivyo na malengo hivyo kile ambacho wamepanga kimenifanya kuweza kuwa hapa na malengo yao ni mazuri,”.
Beki huyo alitambulishwa jana Julai 22 na alianza mazoezi na timu hiyo ambayo imeweka kambi nchini Misri.