MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Yanga leo wanaanza kambi yao rasmi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2022/23.
Yanga chini ya Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi inaanza kambi hiyo ya ndani baada ya ule mpango wa kuweka kambi yao nchini Tunissia kusitishwa.
Awali kambi yao ilitarajiwa kuwa nchini Tunissia lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na muda kuwa mdogo pamoja na likizo ambayo walikuwa wamepewa wachezaji wakaamua kubaki Bongo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wataweka kambi ya ndani na maalumu kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23.
“Tupo imara na kambi yetu itakuwa Kigamboni hasa kutokana na wachezaji wetu kupewa likizo jambo ambalo linaonesha kwamba hatukuwa tukijali lakini ukweli ni kwamba tunajali na wachezaji walipewa mapumziko kwa muda.
“Hata hivyo kumbuka kwamba tulikuwa tuna msimu mrefu na wachezaji ni wafanyakazi hivyo wanawajibu wa kupata mapumziko,”
Miongoni mwa wachezaji ambao waliondoka Bongo ni pamoja na Fiston Mayele aliyetupia mabao 16,Djuma Shaban,Yanick Bangala ambaye ni MVP.