PAPE AWAOMBA MASHABIKI WAZIDI KUMPIGIA KURA

KIUNGO wa Simba, Pape Sakho amewaomba mashabiki na kila mmoja kuendelea na zoezi la kumpigia kura kwenye kipengele ambacho amechaguliwa kuwania tuzo ya bao bora la mwaka la CAF.

Nyota huyo alifunga bao kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ambapo alipachika bao hilo kwa mtindo wa tik taka, ilikuwa ni Uwanja wa Mkapa.

Kwa sasa Simba imeweka kambi nchini Misri kwa ajili ya msimu wa 2022/23 naye ni miongoni mwa wachezaji waliopo kambini chini ya Kocha Mkuu, Zoran Maki.

Pape amesema:-“Nina furaha sana kuwa kwenye kipengele hiki, ni mara yangu ya kwanza,asanteni sababu kuna watu wengi tayari wameanza kupiga kura. Nawaomba tuendelee kupiga kura, tuzo ni muhimu kwa klabu na kwa maisha yangu ya soka hivyo tuendelee kupiga kura.

“Furaha yangu pia ni kubwa kwani kuwa katika orodha pia ni jambo kubwa hivyo nina amini kwamba hili litakuwa kwa ajili yetu na mashabiki kiujumla,” .

Mpigie kura Sakho kupitia http://cafawards2022-goty.com