AZAM FC KAMBI YAANZA RASMI

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa leo itakuwa ni siku rasmi ya mastaa wao kuweza kuanza kambi ya ndani kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yataanza nyumbani kabla ya safari ya kuelekea Misri.

“Tutaanza na kambi ya nyumbani,Jumanne ambapo wachezaji waliopo pamoja na makocha wetu wapya nao watakuwa kwenye maandalizi yetu ya msimu ujao.

“Julai 22 tunatarajia kuweza kuanza safari yetu kuelekea Misri ambapo tutakuwa huko mpaka Agosti na tutatumia siku 20 ampabopo tutarejea kuendelea na maandalizi ya mechi zetu zitakazokuwa zinatukabili.

“Kwa upande wa usajili asilimia kubwa tumekamilisha na ni nafasi moja imebaki ya beki ambaye atatambulishwa utaratibu ukiwa tayari,” amesema Zakaria.

Tayari beki huyo ametambulishwa leo ambaye ni raia wa Senegal anaitwa Malickou Ndoye, akitokea Teungueth FC ya Senegal.