KAMBI POPOTE,TUWAPE WAZAWA MAJINA MAZURI

WAKATI timu kwa sasa zikipambana kusajili wachezaji na kushindana sehemu ya kuweka kambi ulikuwa muda sahihi wa kutambulisha uzi mpya wa msimu wa 2022/23

 

Kuweka kambi nje ya Tanzania ama ndani ya Tanzania sio jambo kubwa ila unafanya hivyo kwa malengo yapi hapo ni msingi muhim kuzingatiwa.

Ndani ya Tanzania kuna sehemu nzuri na tulivu kwa ajili ya kambi tena sehemu ambazo hata ligi haichezwi ingekuwa fursa kwa timu kuweza kuwa karibu na mashabiki wao.

 
Haina maana kwamba ninazuia timu kuweka kami nje ya nchi hapana kila kitu ni mipango ndani ya timu hivyo wanachofanya wao kwa ajili yao na mashabiki wao ni sawa.
 
Mifano ipo tunaona namna ambavyo msimu uliopita mabingwa wa ligi Yanga kambi yao nje ya nchi ilivyoweza kuwa na mvutano mkubwa mpaka Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi alivyobainisha kwamba hakuna jambo ambalo alifanya katika maandalizi ya awali.
 
Mwisho wa siku aliweza kufanikiwa kuwarejesha wachezaji kwenye ubora kwa muda mfupi akiwa Bongo na mambo yakaenda vizuri mpaka wanatwaa ubingwa hawajaonja ladha ya kupoteza pointi tatu nyumbani ama ugenini.
 
Ukweli ni kwamba kambi ya kwanza inaanza kwa mchezaji mwenyewe kisha mazingira yanakuja kuamua kipi ni kipi hivyo hakuna sababu ya kuwaandama wale ambao hawajaweka kambi nje ya nchi.
 

Hali halisi ya bajeti za timu zetu tunazitambua kwamba mambo bado hivyo acha zijipange ndani kisha zikiwa sawa zinaweza kutoka na kufanya kambi matata kwa wakati ujao.

Kuwa nje pia ni wakati wa kufungua ukurasa wa marafiki kimataifa lakini haina ulazima sana.

Kwa wale amao wataweka kambi nje ya nchi Bomba kwa wale watakaoweka kambi ndani ya nchi Fureshi Agosti ipo njiani ni muda wa kuwabadilishia majina wachezaji wazawa hapo VP?

Katika hili naona sio sawa kweli mchezaji awe punda halafu mzawa,ikiwa mgeni utasikia mwenye uwezo wa ajabu nyienyie ni muda wa kuwapa majina yanayowafaa kwa ajili ya kufanya kile kitu kizuri.

Imeandikwa na Dizo Click