BEKI YASSIN AJIUNGA NA SINGIDA BIG STARS

 YASSIN Mustapha leo Julai 18,2022 ameweza kutambulishwa kuwa ni mali ya Klabu ya Singida Big Stars.

Beki huyo msimu wa 2021/22 alikuwa anakipiga ndani ya mabingwa wa ligi ambao ni Yanga.

Ni dili la miaka miwili ameweza kusaini kuweza kupata changamoto mpya katika timu mpya ambayo atakuwa anacheza kwa msimu ujao.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Singida Big Stars,Hussein Massanza ameweka wazi kuwa lengo la kuinasa saini ya beki huyo ni kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

“Malengo yetu ni kuona kwamba kikosi kinakuwa imara kwa ajili ya msimu ujao na kila kitu kinakwenda sawa hivyo ni suala la kusubiri na kuona,”