HESABU ZA USIKU WA TUZO ZIMEGOTA UKINGONI,HESABU ZINAHITAJIKA

USIKU wa tuzo umekwisha, ule usiku wa mastaa umefika kikomo hivyo mwisho wa jambo moja ni mwanzo wa jambo lingine kubwa na gumu zaidi.

Tunaona kwamba kila mmoja amepata kile ambacho amestahili baada ya ushindani kuwa mkubwa kwenye kila hatua.

Makosa ambayo yametokea nina amini kwamba yatafanyiwa kazi hasa kwenye ratiba za tuzo pamoja na mechi za mwisho za kumaliza ligi na fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kwa muda ambao umebaki na ligi kuweza kufika tamati maana yake ni kwamba unakuja msimu mpya mwingine tena ambao utakuwa na ushindani mkubwa zaidi.

Zile ambazo zilikuwa zinapambana kubaki kwenye ligi tunaona kwamba Mtibwa Sugar wao kwenye mchezo wa mtoano wamepenya bado Tanzania Prisons na JKT ambao wanapambana kuona nani atakuwa nani hawa tunawatakia kila la kheri.

Maandalizi tunaona kwa sasa yameanza hasa kwa upande wa usajili ambapo kila timu inahitaji kufanya jambo kwa ajili ya msimu ujao.

Ni umakini mkubwa unahitajika na kila mmoja kufanya mambo yake bila presha kwa kuwa suala la usajili ni suala ambalo linahusu mafanikio ya timu kiujumla.

Kwa wachezaji wazuri watapata kile ambacho wanastahili hivyo wengine wanapata changamoto mpya na wengine wanaondoka kwenye timu zao hilo lipo wazi kwa sasa.

Unapozungumzia mchezaji maisha yake yeye ni mpira na anahitaji kufanya maisha kupitia mpira inapotokea anapata changamoto mpya ni wakati wake wa kuweza kuonyesha ubora zaidi.

Ili uweze kuingia sokoni ni lazima uwe umefanya jambo ambalo litawafanya mabosi na viongozi wa timu waweze kuzungumza nawe ili wawe nawe kwenye kikosi chao kwa msimu ujao.

Uwekezaji mzuri unahitajika kwa timu zote ili kuweza kupata matokeo chanya kwa msimu ujao kwenye mechi zote za ligi na mashindano mengine ya kimataifa.

Namna ambavyo mwendo wa ligi umekwenda na sasa ni muda wakufanya usajili na maandalizi ya msimu ujao kwa kuwa msimu wa 2021/22 umegota ukingoni.

Kwa kila timu nina amini kwamba imeona yale mapungufu ambayo yalikuwa kwenye kikosi hivyo usajili utazingatia yale makosa na kusajili wachezaji wazuri zaidi.

Ukizingatia kwamba ratiba ya ligi imeshatolewa hasa kwa mechi za mwanzo pamoja na ile ya Ngao ya Jamii huku Agosti ikiwa ni muda wa ligi kuanza ni muda mfupi umebaki.

Kwa timu ambazo zimeshuka daraja ni muda wao kufanya maandalizi kwa ajili ya wakati ujao kwa kuwa nafasi ipo.

Kama waliweza kupanda sasa wameweza kushuka na wana nafasi nyingine ya kuweza kurejea kwenye ligi kwa msimu ujao ikiwa mipango itakweda kwa umakini.

Ambazo zimepanda pongezi kwa mara nyingine tena lakini wanapaswa kuelewa kwamba maisha ya kwenye ligi ushindani ni kila siku.

Ikiwa watakuja na hesabu ambazo wametoka nazo kule ndani ya Championship wanaweza kukwama kwa kuwa mbinu huku ni tofauti kabisa.

Hivyo ambacho wanatakiwa kufanya ni kuwa na wachezaji wenye uzoefu,benchi lenye uwezo wa kusoma mchezo na kubadili mbinu haraka zaidi.

Kwenye kila hatua kikubwa ni maandalizi mazuri na wachezaji kuwa tayari kwa ajili ya uleta ushindani wakati ujao kwenye mashindano.

Ikiwa maandalizi yatakuwa ni hafifu leo maana yake ni kwamba kesho hakutakuwa na matokeo mazuri kwa timu ambazo zitacheza kusaka ushindi.

Mashabiki mnastahili pongezi na mzidi kuwa bega kwa began a timu wakati zinacheza ili kuweza kuongeza ilemorali ya kupata matokeo na kuachana na masuala ya ugomvi na fujo hayo sio maisha ya mpira.