KIUNGO MPYA SIMBA ACHEKELEA DILI JIPYA

 VICTOR Akpan kiungo mpya ndani ya Simba amesema kuwa ni furaha kwake kuwa kuwa katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Akpan ametambulishwa rasmi ndani ya Simba, jana Julai 10,2022 kwa dili la miaka miwili ambapo aliibuka hapo akitokea Coastal Union.

Kiungo huyo ameweka bayana kwamba ni ndoto za wachezaji wengi kucheza Simba hivyo naye ndoto yake imetimia.

“Ni ndoto ya wachezaji wengi kucheza Simba kwa sababu Simba ni timu kubwa nami ninajiunga na timu kubwa kwa ajili ya mafanikio.

“Ninaamini kwamba tutafanya mambo mengi mazuri kwa kushirikiana na wengine hivyo ni wakati wetu hasa ukizingatia kwamba nina uwezo na uzoefu,” amesema.

Akpan ni raia wa Nigeria anajiunga na timu hiyo akiwa ni mchezaji wa tatu kuweza kutangazwa rasmi Simba baada ya Moses Phiri na Habib Kyombo kutambulishwa.