KIUNGO MNIGERIA ATAMBULISHWA RASMI SIMBA

KIUNGO wa katikati ya dimba mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mechi za aina zote leo Julai 10,2022 ametambulishwa ndani ya Simba

Ni Victor Akpan raia wa Nigeria ambaye alikuwa nyota wa kikosi cha Coastal Union ya Tanga.

Hivyo msimu ujao atakuwa ndani ya mabingwa mara nne mfululizo wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba.

Kiungo huyo alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu,Juma Mgunda ambaye wanamuita Pep Guardiola Mnene.