IKIWA leo Julai 9,2022 siku ya uchaguzi wa Yanga ambao unafanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,mgombea pekee wa nafasi ya Urais Injinia Hersi Said amezungumzua vipaumbele vyake.
Vipaumbele vyake ni pamoja na:-
1. Miundombinu ya Klabu ya Yanga.
a. Ujenzi wa uwanja wa mechi wenye uwezo wa kubeba watu 20,000 – KAUNDA JANGWANI
b. Marekebisho ya jengo la klabu – JANGWANI
c. Kuendeleza TRAINING CENTRE – KIGAMBONI
2. Mabadiliko ya muundo wa klabu
Klabu yetu kupitia kwa wanachama walipitisha mfumo wa mabadiliko. Nikiwa mmoja waumini wa mabadiliko hayo, naahidi kuyasimamia na kuyaendeleza mabadiliko hayo kwa mujibu wa katiba yetu.
3. Kuimarisha uchumi wa klabu.
Kupitia kwa miradi ya usajili wa wanachana.
Kupitia kwa miradi ya usajili wa washabiki
Kuvutia Wadhamini mbali mbali.
Kuvutia wawekezaji.
4. Kujenga kikosi imara cha kuleta mataji na ushindani.
a. Ligi Kuu
b. FA Cup
c. Ngao ya Jamii
d. Mashindano ya kimataifa
5. Kujenga timu imara za wanawake na vijana
a. U-17
b. U-20
c. Yanga Princess
6. Kuongeza ushirikiano baina ya klabu na wanachama na mashabiki wake, wadau mbali mbali ikiwemo idara za serekali, sekta binafsi, waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla.
Mwanachama wa Young Africans SC kwa heshima na taadhima naomba kura yako ya ndio amesema Eng. Hersi Said Mgombea Urais.