HUYU HAPA MVP LIGI KUU BARA 2021/22

KATIKA usiku wa tuzo za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 uliweza kukamilika kwa kila mmoja kuweza kujua kile ambacho amekivuna.

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa umakini ilikwenda kwa kiungo wa Yanga, Yannick Bangala.

Tuzo hiyo ilitolewa na mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa alimkabidhi tuzo ya mchezaji bora msimu wa 2021/22,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha kwa niaba ya Yanick Bangala ambaye ni MVP.

Bangala alikuwa anawania tuzo hiyo akipambanishwa na nyota wengine wawili ambao walikuwa nao wapo kwenye kipengele hicho kwa msimu wa 2021/22.

Ni Mayele ambaye ni mshambuliaji yeye ni mali ya Yanga pamoja na Henock Inonga ambaye ni mali ya Simba.

Pia wachezaji wote hawa watatu wapo kwenye kikosi bora kwa msimu wa 2021/22 ambao Yanga ni mabingwa.

Tuzo hizo zilifanyika usiku wa kuamkia leo Julai 8 kwenye Ukumbi wa Hotel ya Rotana.