HAJI MANARA AOMBA MSAMAHA KWA RAIS WA TFF

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amemuomba msamaha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Wallace Karia kutokana na tukio lililotokea Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Ofisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo  Julai 5,Manara amenukuliwa akisema:

“Rais nimekuja kwa kukujibu vile au kujibizana mimi na wewe nimekosea “I’m Sorry” mi ni mdogo wako mimi ni kama mwanao, No matter labda wewe ndiye uliyeanza lakini kukujibu tu hata kama ulinianza nimekosea, I’m Sorry My President of Football.” Amesema Manara.

Aidha Manara ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka nchini ambao wanaona kwa kujibu vile alikosea akisema yeye ingawa amekaa kwenye masuala ya soka kwa muda mrefu lakini anabaki kuwa binadamu pia hivyo anaomba msamaha.