FRED Felix Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold, amebainisha wazi sababu kubwa ya mshambuliaji George Mpole kufunga mabao 17 ni kutimiza majukumu aliyopewa.
Mpole ni mzawa aliyeibuka kinara wa mabao Ligi Kuu Bara 2021/22 akimpoteza Fiston Mayele wa Yanga raia wa DR Congo mwenye mabao 16.
Akizungumza na Spoti Xtra, Minziro alisema: “Tulikuwa tunahitaji pointi tatu kwenye mechi zetu, ili uzipate ni lazima ufunge mabao, hicho ndicho ambacho alikuwa anafanya Mpole akishirikiana na wenzake.
“Kuanzia kwenye uwanja wa mazoezi, huko mipango ilikuwa inapangwa na furaha yetu ni kuona kila mchezaji anafanya vizuri, mwisho wa siku tunaona kafanya kile ambacho amekifanya ni furaha kwa kila mmoja.”