MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Misri Mohamed Salah ameongeza mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kubakia katika klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya mersesyde.
Salah amesaini mkataba huo unaotarajiwa kumalizika majira ya kiangazi mwaka 2025 huku akipokea kitita cha Paundi 350,000 ambayo ni sawa na zaidi ya Milioni 982 kwa wiki za kitanzania
Kwa mkataba huo mpya Salah anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupokea mshahara mkubwa katika historia ya klabu hiyo.
“Najisikia furaha na natarajia kuchukua makombe na klabu hii, ni siku nzuri kwa kila mtu.” Alisema Salah
“Inachukua muda kidogo kuongeza mkataba lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa inabidi tufikirie yajayo, nadhani mnaweza kuona kwa kipindi cha miaka mitano ahdi sita timu imekuwa ikifanya vizuri. Msimu uliopita ilibaki kidogo tu tuchukue makombe manne lakini ndani ya wiki ya mwisho tukapoteza makombe mawili.
“Nadhani tupo katika nafasi ya kupambana kwa kila kitu. Tuna usajili mpya pia. Tunachotakiwa ni kuendelea kufanya kazi kwa bidii tuna maono mazuri na tupambanie kila kitu tena.”
Salah alijiunga na Liverpoo mwaka 2017 akitokea katika klabu ya AS Roma ambapo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 44 katika msimu wake wa kwanza kwa sasa ana umri wa miaka 30.