NYAKATI za mashaka kwa sasa kwa baadhi ya timu na mashabiki ni sasa hasa kutokana na kushindwa kupata matokeo kwenye mechi ambazo walicheza mzunguko wa kwanza.
Ukurasa wa mwisho kwa mechi ambazo zitachezwa utaamua nani atakuwa nani baada ya mwisho wa msimu kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu.
Mbeya Kwanza asanteni kwa kuja nadhani kwamba mlipata kile ambacho mlistahili na mnakwenda kujipanga upya kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa.
Hamna namna ilikuwa ni lazima timu kushuka kama ambavyo timu zinapanda kwa kuwa ni mwanzo wa msimu yote yalikuwa wazi na sasa ni hatua ya mwisho.
Ngoma acha iendelee kupigwa hasa kutokana na ushindani ambao umekuwepo ndani ya ligi msimu huu katika hilo kila timu zinahitaji kupewa pongezi.
Hata kwa kushindwa kufikia malengo kwa kuwa walishapanga malengo basi ni moja ya jambo ambalo linastahili pongezi kwa kila timu.
Wachezaji wamefanya kazi kubwa na sasa wanakwenda kumaliza kile ambacho walianza nacho kwa msimu huu wa 2021/22 ipo wazi katika hilo.
Kwa wale ambao wameshindwa kufanya sawa na kile ambacho walitarajia ni wakati wao kuweza kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao.
Makosa yapo huwezi kuyaepuka lakini ambacho kinapaswa kuchukuliwa ni namna ya kuweza kuyatatua na kuendelea na maisha.
Kwenye mechi za mwisho huwa kunakuwa na masuala ya fitina na upangaji wa matokeo hili lisipewe nafasi, atakayeshinda ni yule ambaye amejipanga.
Mpira unahitaji maandalizi mazuri na mipango makini kwa ajili ya kupata matokeo na kila timu ambayo itakwama kujipanga basi itafanikiwa kushindwa.
Kila timu iweke kando ile mipango ya kuhitaji kupanga matokeo ili kuweza kubaki ndani ya ligi ama kushuka kila mmoja na avune kile anachostahili.
Muda mrefu wa mzunguko wa kwanza tuliambiana kwamba mipango yote inabidi ianze mwanzo hivyo mwisho wa msimu ni muda wa kumalizia mipango ambayo ilianza kupangwa mwanzo.
Yote kwa yote kila mmoja anapenda kupata matokeo mazuri na matokeo hayo hayaji bila jitihada kwa kila mmoja kufanya vizuri.
Maandalizi yanaanza kwenye mazoezi kabla ya mechi na siku ya mchezo ni kukamilisha kile ambacho umejifunza kwenye mazoezi,kazi inakuwa imefika ukingoni.
Ambacho kinaendelea kwa sasa ni mwendo wa matokeo wa kile ambacho kilianza kufanyika msimu uliopita,hakuna namna ni jambo la kukubali na kufanyia kazi.
Hakuna ambacho kinashindikana kwenye mpira ikiwa kutakuwa na mipango makini hivyo mechi za mwisho wa msimu ziwe ni kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wa waamuzi ninapenda kuwapa pongezi kwa wale ambao walifanya kazi yao kwa umakini kwenye kutafsri sheria 17 za mpira.
Wamefanya kazi kubwa na ngumu kwa mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili ambao unakwenda kufika ukingoni hapo pongezi wanastahili.
Kwa msimu ujao ambao ni mpya ni muhimu kuja na majibu ya yale maswali ambayo yalikuwa magumu kujibika kwa wakati huu, kila la kheri.