WINGA HUYU ATUA BONGO,ATAJWA KUIBUKIA SIMBA

 WINGA, Harrison Mwendwa ametua Dar es Salaam leo Juni 24 ambapo anatajwa kuwa amekuja kukamilisha suala la usajili wake na timu moja inayosiriki Ligi Kuu Bara.

Winga huyo anatajwa kuingia kwenye rada za Azam FC,Yanga na Simba ambazo zinahitaji kuweza kupata saini yake kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23.

Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto na aliwahi kucheza kwenye kikosi cha Mathare United,Kariobagi Sharks na AFC Leopards kwenye soka la ushindani.

Kwa sasa nyota huyo ni mchezaji huru ambapo chapuo kubwa wanapewa kuinasa saini yake ni Simba inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola