KIUNGO WA YANGA FEI AWEKA WAZI SABABU ZA UPAMBANAJI

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ameweka wazi kuwa kazi kubwa ambayo wanaifanya uwanjani ni kusaka ushindi jambo linalowafanya wawe na furaha.

Fei ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amekuwa kwenye ubora kila awapo uwanjani.

Kesho Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City na wanatarajiwa pia kukabidhiwa taji lao la ligi ambalo litakuwa ni la 28.

Kiungo huyo amesema:”Kikubwa ni kuona tunapata matokeo kwani kila mchezo kwetu ni mgumu na tunafurahi kila mara tunaposhinda.

“Mashabiki wamekuwa nasi kwenye mechi zote hilo limetup nguvu hivyo wao nao ni sehemu ya mafanikio yetu kwenye mechi ambazo tunacheza,”.

Kiungo huyo ametoa jumla ya pasi nne kwenye ligi msimu huu wa 2021/22.