PASCAL Wawa beki wa kati wa Simba leo ameagwa rasmi na mabosi hao kwa kuweka wazi kuwa hataongezewa mkataba mwingine.
Taarifa iliyotolewa na Simba leo Juni 21,2022 imeeleza namna hii:”Baada ya kutumikia timu yetu kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao.
“Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho,”