NYOTA MPYA YANGA AOMBA JEZI NAMBA 7

LAZAROUS Kambole mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anapenda kutumia jezi namba 7 kwa msimu mpya wa 2022/23.

Raia huyo wa Zambia amesaini dili jipya ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Alitambulishwa ndani ya kikosi hicho Juni 16,2022 ikiwa ni siku moja baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa 28 wa ligi.

Namba hiyo 7 ndani ya kikosi hicho kwa sasa inatumiwa na Balama Mapinduzi ambaye amekuwa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

“Ninapenda jezi namba saba kwa kuwa nimekuwa nikiivaa hiyo mara kwa mara kwenye timu ya taifa ambapo nilikuwa nikifanya vema ikishindikana basi nitavaa nyingine, amesema”