PASI ZA BWALYA SIMBA KAMA DAKIKA ZAKE

RALLY Bwalya, mchezo wake wa kuagwa na mabosi zake Simba ilikuwa mbele ya KMC alitumia dk 88 na alipiga pasi 88 kati ya hizo mbili hazikuwafikia walengwa na muelekeo wake ulikuwa ni kwa Pape Sakho.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 19 na Simba iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ambapo watupiaji walikuwa ni Pape Sakho, Henock Inonga na Kibu Dennis.

Kwa upande wa KMC wao bao lao lilifungwa na Hassan Kabunda ambaye alikuwa wa kwanza kufunga kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Bwalya ambaye anatajwa kuibukia Klabu ya Amazulu ya Afrika Kusini aliibuka ndani ya kikosi cha Simba akitokea Power Dynamo ya Zambia.

Nafasi yake ilichukuliwa na Yusuph Mhilu ambaye aliingia baada ya Bwalya ambaye jezi yake mgongoni ni namba 8 aliweza kuelekea benchi.

Msimu huu amecheza jumla ya mechi 19 ndani ya ligi na kufunga bao moja na kutengeneza jumla ya pasi tatu za mabao.