SIMBA YAPINDUA MEZA MBELE YA KMC

KWENYE mchezo wa Ligi Kuu Bara leo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, kikosi cha Simba kimeweza kupindua meza mbele ya KMC.

Pia mchezo wa leo ambao ni wa mzunguko wa pili umetumika kwa ajili ya kumuaga mchezaji wao Rally Bwalya ambaye amecheza mechi 19 na kutoa pasi tatu za mabao kuweza kuagwa kwa kuwa amepata timu nyingine.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 3-1 KMC ambao wao walianza kupachika bao la kuongoza.

Ilikuwa dk ya 41 kupitia kwa Hassan Kabunda ambaye alitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba chini ya Inonga.

Kwa upande wa Simba iliweza kufunga mabao yote matatu kipindi cha pili ilikuwa ni kupitia kwa Kibu Dennis dk ya 52, Pape Sakho dk ya 62 na Henock Inonga alipachika bao la tatu dk ya 66.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 za ligi msimu wa 2021/22 ambapo mabingwa ni Yanga.