KOCHA ANAYETAJWA KUIBUKIA SIMBA AFUNGUKA

INAELEZWA kuwa aliyekuwa kocha wa Kaizer Chiefs na kutimuliwa kabla ya mkataba wake kuisha Stuart Baxter raia wa Uingereza (68), April 24, 2022 alifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Baxter alikutana na Barbara jijini Johannesburg Simba ilipoenda kucheza na Orlando Pirates mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kocha huyo amesema kikao hicho kilikuwa kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo.

“Nilikuwa na mazungumzo kadhaa ndani ya nchi katika Ligi Kuu ya Soka na barani, ikiwa ni pamoja na kukutana na Simba,” Baxter sasa ameiambia SABC Sport.

“Lakini nadhani ni muhimu kusahihisha habari fulani. Nilichukua kikao na Simba kujadili mipango yao kwenda mbele na ninahisi sasa kuna mawakala wanaozungumzia hili.

“Bado sijaamua kama kutakuwa na mazungumzo zaidi na klabu yoyote ambayo nimekutana nayo. Lakini mpira wa miguu ni wakati, kwa hivyo tusubiri tuone,” alisema.

Muingereza huyo aliachana na Amakhosi mwezi Aprili wakati bado alikuwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Alipotafutwa Barbara ili aweze kuzungumzia jambo hilo amesema kuwa yupo kwenye kikao.