KIUNGO wa Klabu ya Simba, Rally Bwalya atasepa ndani ya kikosi hicho baada ya mabosi wa timu hiyo kuweka wazi kwamba wamefikia makubaliano na timu moja iliyokuwa inahitaji saini yake.
Simba wameweka wazi kuwa wanashukuru kwa huduma ya kiungo huyo raia wa Zambia ambaye alitua hapo Agosti 2020 akitokea Klabu ya Power Dynamo.
Ni dili la miaka mitatu alisaini hivyo anauzwa akiwa amebakisha kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia Simba.
Jumapili kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC Uwanja wa Mkapa kiungo huyo ataagwa rasmi.
Inaelezwa kuwa Klabu ya Amazulu ya Afrika Kusini imempa kandarasi ya miaka miwili.