IMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Abdul Suleiman, ‘Sopu’ yupo kwenye rada za Yanga na Simba ambao wanawania saini yake.
Nyota huyo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Coastal Union akiwa ametupia mabao 7 ndani ya ligi na ni namba moja kwenye timu hiyo.
Habari zimeeleza kuwa Simba wanahitaji kuipata saini ya nyota huyo ambaye aliwahi kucheza kwenye timu hiyo kabla ya kwenda kwa mkopo Ndanda na kujiunga na Coastal Union.
“Baada ya kuweza kujiunga na timu ya Ndanda aliweza kwenda Coastal Union sasa Simba wanahitaji huduma yake na Yanga pia wameulizia dili la kumpata nyota huyo,” ilieleza taarifa hiyo.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa watafanya usajili makini wa kitaifa na kimataifa.