SIMBA YALIPA KISASI UWANJA WA MKAPA

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya Mbeya City ni muhimu kwao katika kuongeza hali ya kujiamini kwa mechi zijazo.

Ushindi huo ni kisasi kwa Simba ambao walinyooshwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza na kuacha pointi tatu mazima mbele ya Mbeya City.

Jana Juni 16, Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Matola kukaa benchi baada ya Pablo Franco ambaye alikuwa Kocha Mkuu, kuchimbishwa hapo.

Watupiaji kwenye mchezo huo walikuwa ni Pape Sakho aliyepachika mabao mawili ilikuwa dk ya 39 kwa mkwaju wa penalti na dk ya 55 huku bao moja likifungwa na Peter Banda ilikuwa dk ya 77.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kujikita nafasi ya pili n pointi 54 huku ile ya kwanza ikiwa mikononi mwa mabingwa Yanga wenye pointi 67.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Paul Nonga aliyeweza kumtungua Aishi Manula.

Matola amesema:”Ulikuwa ni mchezao mzuri na ambacho tulikuwa tunahitaji ni ushindi kwenye mechi yetu muhimu hivyo kikubwa ni kuezidi kuendelea kujipanga kwa mechi zijazo,”.