KIUNGO Victor Akpan mali ya Coastal Union anatajwa kuwavuruga vigogo ambao wanawania saini yake kwa sasa.
Ni Simba walianza kuiwania saini ya kiungo huyo ambaye jana mbele ya Yanga aliweza kutimiza majukumu yake kwa umakini licha ya timu hiyo kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0.
Habari zinaeleza kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kumnasa kiungo huyo raia wa Nigeria kwa kuwa mazungumzo yamekwenda vizuri ila kilichobaki ni kukamilisha masuala madogo ya usajili.
Baada ya Simba kuwa kwenye mazungumzo na kiungo huyo inatajwa kuwa Azam FC, Yanga nao wanamvutia kasi kiungo huyo ili waweze kupata saini yake.
Simba inahitaji kuimarisha kikosi chake kwa sasa ikiwa imeshamtambulisha Moses Phiri na inahitaji kuongeza nguvu zaidi kuwa tofauti kwa ajili ya msimu ujao baada ya kupoteza ubingwa wa ligi ambao umekwenda Yanga.