MWAMBA HUYU HAPA KUTUA YANGA,YEYE NI BEKI

IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota Joyce Lomalisa ambaye anakipiga Klabu ya Sagrada Esperanca ya Angola.

Nyota huyo ni beki ambaye anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Hivyo kutua kwake ndani ya Yanga kutafanya aweze kuungana na beki mwingine wa kazi, Yannick Bangala ambaye amekuwa imara kwenye ulinzi.

Tayari Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 15,2022 kwa kufikisha pointi 67 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wana mpango wa kusajili wachezaji wa kimataifa kwa ajili ya mechi za kimataifa ikiwa ni kutoka nchi mbalimbali kama Angola,Afrika Kusini pamoja na nchi nyingine.