VIWANJA VINNE KUJENGWA SIMBA,MPANGO KAZI UPO HIVI

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wana mpango wa kuwa na viwanja vinne kwenye eneo la Simba Mo Arena,Bunju kwa ajili ya matumizi ya timu hiyo.

Jana, Barbara aliongozana na  msanifu majengo, (Architect) eneo la Bunju kukagua mipaka ya eneo ambalo litatumika kwenye ujenzi kabla ya Bodi ya Wakurugenzi kukutana Ijumaa ili kumpitisha mkandarasi ambaye atajenga uwanja.

Barbara amesema: “Kuna vitu tumeongeza na asilimia 90 duniani viwanja vinavyochezwa ni vya asili na tunataka kuwa na pitch tatu za asili, (kwa sasa Bunju kuna uwanja mmoja wa asili na mmoja wa nyasi bandia) na moja ya nyasi bandia na tunataka kutengeneza sehemu ya kukaa hata watu 5,000 kwa ajili ya timu ya vijana na Wanawake.

“Tumezunguka eneo lote ambalo ni kubwa na Ijumaa bodi inakaa kuweza kujadili proposal, (kazi mradi) na tulianzisha kampeni mwezi wa 12  tumeanza tunaweza unakumbuka? Wanasimba walichangia na awamu ya pili ilikuwa nani zaidi pamoja na Azam TV lengo ni kuweza kuendeleza Mo Simba Arena.

“Miezi miwili tumetumia kupitia michoro na ili uwe na viwanja lazima uwe na sehemu ya vijana kukaa,GYM,Swimming pool, sehemu ya timu ya nyumbani na ugenini kukaa na sehemu ya benchi la ufundi na vifaa vyote vya viwanja vikubwa.

“Nimeenda Qatar kuangalia viwanja vya Kombe la Dunia, Mwenyekiti Murtanza Mangungu naye tulimpeleka Uturuki kuangalia viwanja, huwezi kuwa na viwanja bila kuwa na training facilities,hiki ni kitu cha kwanza na kikao cha bodi kilinipa kazi ya kufanya ili kupeleka proposal ambayo itachambuliwa na bodi.

“Bodi wakipitisha utaona nini kitaendelea na wakitoa ruhusa sisi tutaendelea,changamoto kubwa ni namna ya kujenga ukuta ambao unaweza kugharimu milioni mia mbili na uwanja huu ni mkubwa,pia kuna watu ambao wapo ndani ya eneo hili,” alisema Barbara.