YANGA YATUPA DONGO KIMTINDO SIMBA

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amewapiga dongo kiaina wapinzani wao Simba kwa kubainisha kwamba mashabiki wa timu iliyoshinda wanapaswa kuamka mapema wengine saa 7 mchana.

Yanga Mei 28 iliweza kuwatungua watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, Uwanja wa CCM Kirumba.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Feisal Salum ilikuwa dk ya 25 kwa shuti la mguu wa kulia akiwa nje ya 18 likamshinda Beno Kakolanya.

Manara amesema:”Mashabiki wa Yanga mnapaswa kuamka saa tatu mapema asubuhi na kuweza kuipokea timu ikirejea uwanja wa ndege kwa wale wa Dar.

“Mashabiki wa timu zingine hizo, (Simba) nyie laleni kuamka saa 7 na kuendelea, ila Wananchi, (Yanga) kesho msiende kazini,mkiulizwa semeni Bugati katuambia Yanga bingwa,akibisha mpe kibao,”.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwasili leo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kumaliza mzunguko wa pili wa 2021/22.