REAL Madrid wametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitungua bao 1-0 Liverpool kwenye mchezo wa hatua ya fainali iliyochezwa Uwanja wa de France.
Licha ya Liverpool kuwa na matumaini ya kuweza kulipa kisasi cha mwaka 2018 walipokutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid kuweza kushinda bado wakati huu wameshindwa kwa mara nyingine tena.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Vinicius Junior ilikuwa dk ya 59 lilitosha kuwahakikishia ubingwa Real Madrid.
Rekodi zinaonyesha kuwa Real Marid waliweza kupiga mashuti mawili pekee ambayo yalilenga lango huku Liverpool ikipiga jumla ya mashuti 9 ambayo yalilenga lango.
Mchezo huo ulichelewa kuanza kutokana na sababu ya mashabiki wa Liverpool kuwa kwenye kashkashi wakati wa kuingia ndani ya uwanja kuweza kushuhudia mchezo huo jambo lililofanya uweze kuchelewa kuanza.