PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema wanajua mechi ya leo nusu fainali Kombe la Shirikisho itakuwa ngumu ila watajitahidi kutafuta ushindi mbele ya Yanga
Simba ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Kocha Pablo ameweka wazi kwamba maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa nafasi ya kuweza kupata ushindi mbele ya wapinzani wao Yanga.
“Tunajua kwamba tunacheza na timu nzuri na yenye ushindani mkubwa hivyo ambacho tutakifanya ni kujitahidi kuweza kushinda.
“Kila mchezaji yupo tayari na sisi tupo tayari kuona tunapata ushindi, kikubwa ni kuwa tayari kushindana kwani hakuna mashaka na tunajua kwamba nusu fainali huwa inakuwa ngumu,”.
Simba ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Shomari Kapombe nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo vizuri kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata ushindi.