MAKOCHA wawili ambao wanatarajiwa kuongoza vikosi vyao Uwanja wa CCM Kirumba kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho wameibiana mbinu ndani ya dakika 90 kabla ya kukutana uwanjani.
Ni Nasreddine Nabi Kocha Mkuu wa Yanga wa alianza kuweza kuiba mbinu za Pablo Franco Uwanja wa Kirumba baada ya kushuhudia dk 90 za kazi kwenye mchezo uliokamilika kwa Geita Gold 1-1 Simba ilikuwa ni Mei 22.
Kisha Nabi alipopanga kete yake mbele ya Biashara United, Mei 23 Uwanja wa CCM Kirumba, Pablo alikuwa jukwaani akiwachambua wapinzani wake Yanga ambao watakutana nao kwenye mchezo ujao.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze alisema kuwa kila wanapokwenda kucheza na mpinzani wao ni lazima watazame mechi zao zilizopita ili waweze kujua namna ya kumkabli.
“Kila timu ina mbinu zake na kabla ya kwenda kucheza mchezo huwa tunaangalia mechi zilizopita za wapinzani ili kupata mbinu zao ili tujue namna ya kuwakabili,” .