PRISONS WATOSHANA NGUVU NA GEITA GOLD

LICHA ya kuanza kufunga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Tanzania Prisons waliweza kugawana pointi mojamoja na Geita Gold.

Bao la dakika ya 30 lililofungwa na jeremia Juma lilidumu ndani ya kipindi cha kwanza kwa kuwa alifunga dk ya 38 kwa kuwa kuwa kipindi cha pili vijana wa Geita Gold waliweza kuweka usawa.

Ilikuwa kupitia kwa Daniel Lyanga ambaye alipachika bao hilo dk ya 50 na kuwainua mashabiki wa Geita Gold waliojitokeza kushuhudia burudani.

Sasa Prisons inafikisha pointi 25 ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo na Geita Gold wao wapo nafasi ya 5 pointi 36.